Thursday, April 1, 2010

TAMADUNI
















Kama ilivyo kwa watu wengi wanasema kuwa tamaduni za makabila mbalimbali zimekuwa zikipotea lakini kwa wenyeji wa mikoa ya kusini hilo lipo bado sana utokana na mila na tamaduni hizi kuendelezwa, mfano uchongaji wa sanamu (vinyago), ngoma za asili, nyumba za asili, n.k

AJARI ZA BARABARANI






Kwa miaka ya hivi karibuni kuwepo na usafirishaji wa abiria kumezuka wimbi kubwa la ajari za barabarani licha ya serikali kutilia mkazo wa hatua za kufuata juu ya kupunguza matukio haya ya ajari ambapo maelfu ya watu wanapoteza uhai, mali na nguvukazi ya taifa.

USAFIRI WA KUSINI





Tumeona japo hali ya usafiri kwa wananchi wa mikoa hii ya kusini kutokuwa nzuri kwa siku za nyuma hali hiyo inaonyesha kuleta matumaini kwa wasafiri wa kwenda katika mikoa hiyo, mbali na hali ya miundombinu hususani ya barabara kutotengemaa kwa huwepo sehemu korofi. Ambazo kwa jitihada za serikali inajitahidi kulitafutia ufumbuli. Lakini usafir ni wa uhakika kwenda maeneo hayo ya kusini.

HATUA YA UZAAJI WA KOROSHO






Korosho ni zao ambalo linalimwa katika maeneo haya ya mikoa ya kusini. Katika hatua za hawali kabisa wakulima wanaanza kuyaandaa mashamba yao mapema kwa kufanya palizi na kuyasafisha. Inafika hatua ya mikorosho kutoa maua ambapo wakulima hawa hupulizia dawa maalum kwa ajili ya wadudu wahalibifu. Baadae maua haya yanatoa matunda (korosho) hizi zinakuwa changa kwa wenyeji wanaziita (madunge). na katika hatua ya upuliziaji wa dawa hili hufanyika kuanzia mara tatu na zaidi.